Mark 15:43-46

43 aYusufu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na ambaye alikuwa anautarajia Ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Isa. 44Pilato alikuwa akijiuliza kama Isa alikuwa amekwisha kufa. Hivyo akamwita yule jemadari, akamuuliza iwapo Isa alikuwa amekwisha kufa. 45 bBaada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yusufu ruhusa ya kuuchukua huo mwili. 46 cHivyo Yusufu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili kutoka msalabani, akaufunga katika kile kitambaa cha kitani, na kuuweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi.
Copyright information for SwhKC